1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia kusini kwa Gaza

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Ndege za Israel zimeshambulia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Gaza mapema leo, ikiwa ni pamoja na sehemu za kusini ambako Israel ilitangaza maeneo salama.

Gaza Trauernde nach Raketeneinschlag in Ahli Arab Krankenhaus
Mwanamke wa Kipalestina akilia akiwa amebeba mto wa kulali mbele ya jengo la hospitali ya Ahli Arab iliyoshambuliwa. Hamas na jeshi la Israel wanalaumiana kwa mashambulizi hayo ya tarehe 17 Oktoba, ambayo yaliuwa mamia ya watu.Picha: AFP

Mashambulizi hayo yamefanyika hata baada ya Israel kukubali siku ya Jumatano (Oktoba 18) kuiruhusu Misri kupeleka msaada kiasi wa kibinaadamu mjini Gaza, siku 12 tangu ianze kuushambulia ukanda huo na kutangaza mzingiro kamili.

Tangazo la mpango wa kupeleka chakula, maji na mahitaji mengine Gaza limekuja wakati hasira juu ya shambulio baya dhidi ya hospitali mjini Gaza, zikienea kote Mashariki ya Kati.

Soma zaidi: Israel na Hamas zaendelea kushambuliana Ukanda wa Gaza

Rais Joe Biden wa Marekani amerejea Washington baada ya kuizuru Israel siku ya Jumatano katika kile kinachosemwa ni "kujaribu kuzuwia kusambaa kwa mzozo huo."

Watu 3,478 wameuawa mjini Gaza, na zaidi ya 12,000 kujeruhiwa, huku wengine 1,300 wanaaminika kufunikwa na vifusi kulingana na maafisa wa afya wa Gaza tangu Israel ilipoanza operesheni ya kijeshi Oktoba 7.

Kwa upande wake Israel, imeripoti vifo zaidi ya 1,400, na wengine watapato 200 walichukuliwa mateka na wanamgambo wa Hamas baada ya uvamizi wa kundi hilo, ambalo linatambuliwa na Marekani na Umoja wa Ulaya kuwa kigaidi. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW