1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia maeneo ya Hamas kusini mwa Gaza

4 Desemba 2025

Israel imesema imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya wanamgambo wa Hamas kwenye eneo la kusini mwa Gaza, katika kujibu shambulizi lililotokea mapema Jumatano na kuwajeruhi wanajeshi watano wa Israel.

Khan Younis, Ukanda wa Gaza 2025 | Israel imeishutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano ya amani
Majengo yaliyoshambuliwa licha ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigamo kati ya Israel na HamasPicha: Ramadan Abed/REUTERS

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Hamas Jumatano ilikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya wapiganaji wake kutoka kwenye handaki huko Khan Younis na kuwashambulia wanajeshi wa Israel kwenye eneo ambalo wanalidhibiti.

Israel iliishutumu Hamas kwa kukiuka makubaliano ya amani, kabla ya kufanya mashambulizi ya anga ya awali. Hata hivyo, Hamas imetoa taarifa inayolaani vikali mashambulizi hayo ya Israel huko Khan Younis.

Mwili wa mateka mwingine watambuliwa

Wakati huo huo, mabaki ya mwili yaliyokabidhiwa na Hamas kwa Israel yamegundulika kuwa ya mateka raia wa Thailand.

Jeshi la Israel limesema Alhamisi kuwa Sudthisak Rinthalak alitekwa kutoka Israel wakati wa mashambulizi ya Hamas na makundi mengine ya wanamgambo Oktoba 7, mwaka 2023.

Mwili wake umekuwa ukishikiliwa na kundi la Islamic Jihad katika Ukanda wa Gaza. Alifariki Mei 16, 2024 akiwa na umri wa miaka 42.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW