1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia Lebanon kujibu maroketi ya Hezbollah

2 Machi 2026

Israel imeyashambulia maeneo ya kusini mwa mji mkuu wa Lebanon leo alfajiri baada ya kundi lenye mafungamano na Iran la Hezbollah kufyetua droni na maroketi kuelekea Israel.

Lebanon Beirut 2026 | Mashambulizi ya Israel
Moshi ukifuka baada ya mashambulizi ya anga ya Israel kwenye mji mkuu wa Lebanon, Beirut.Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Mashuhuda wamesema zaidi ya mitikisiko 12 ya makombora imesikika mjini Beirut katika mashambulizi yaliyo makali zaidi kufanywa na Israel nchini Lebanon tangu vita vyake na Hezbollah vya mwaka 2024.

Kundi la Hezbollah lenye ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani ya Lebanon limesema limeilenga Israel kwa maroketi na droni ili kuonesha mshikamano na Iran na kulipa kisasi kwa kuuliwa Khamenei.

Ingawa hivi sasa nguvu za kundi hilo zimepungua tangu vita vya mwaka 2024, Israel inasema bado linao uwezo fulani wa kijeshi wa kupanga na kushambulia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW