1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia maeneo 350 ya kijeshi nchini Syria

11 Desemba 2024

Israel imethibitisha kuwa imeshambulia kwa mabomu zaidi ya maeneo 350 ya kijeshi nchini Syria ikilenga maeneo ya kimkakati, meli za kivita na hifadhi za silaha.

Raia wa Syria akishikilia kombora ambalo halikuharibiwa na mashambulizi ya Israel
Raia wa Syria akishikilia kombora ambalo halikuharibiwa na mashambulizi ya IsraelPicha: DELIL SOULEIMAN/AFP/Getty Images

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema  wimbi la mashambulizi hayo ya anga huko Syria ni muhimu ili kuzuia silaha hizo zisitumike dhidi ya Israel kufuatia kuanguka kwa serikali ya rais Bashar al-Assad.

Katika mji mkuu Damascus, hali imerejea kuwa ya kawaida baada ya sherehe za siku tatu huku maduka na benki vikifunguliwa tena. Waziri Mkuu wa mpito Mohammad al-Bachir ametoa wito wa kudumisha hali ya utulivu.

Marekani imetangaza kuwa itatambua na kuunga mkono serikali mpya ya Syria ambayo itaachana na ugaidi, itatokomeza hifadhi za silaha za kemikali na kulinda haki za walio wachache na wanawake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW