1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia "njia za kusafirisha silaha" za Hezbollah

6 Desemba 2024

Jeshi la Israel limesema leo kuwa limefanya mashambulizi kulenga kile walichokiita “njia za usafirishaji wa silaha” za kundi la wanamgambo la Hezbollah katika mpaka wa Syria na Lebanon.

Libanon Beirut | Frau liest den Koran | Ermordung des Hisbollah-Führers Hassan Nasralla
Picha: Hassan Ammar/AP Photo/picture alliance

Mashambulizi hayo yanatokea wiki moja tu baada ya kufikiwa kwa mpango wa kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.

Vyombo vya habari vya Lebanon na Syria vimeripoti kuwa shambulio hilo la anga limelenga kivuko cha mpakani cha Al-Arida, eneo ambalo tayari liliharibiwa vibaya wakati wa vita kati ya Israel na Hezbollah.

Israel yalaumiwa katika ripoti mpya ya Amnesty International

Shirika la habari la serikali ya Syria, SANA limeripoti kuwa kivuko hicho cha mpakani cha Al-Arida hakifanyi kazi tena baada ya kushambuliwa leo Ijumaa. 

Shambulio hilo limefanyika katikakati ya shutma kutoka pande zote mbili, Israel na Hezbollah, za kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano yalioanza kutekelezwa kuanzia Novemba 27, baada ya karibu miezi miwili ya vita kamili kati ya Israel na Hezbollah.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW