1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yashambulia ofisi muhimu za serikali Tehran

3 Machi 2026

Jeshi la anga la Israel limearifu kwamba limefanya mashambulizi yaliyoyalenga majengo muhimu ya serikali katika mji mkuu wa Iran, Tehran. Majengo yaliyoshambuliwa ni pamoja na ikulu.

Tehran, Iran 03.03.2026
Moshi uliotanda baada ya mashambulizi katika mji mkuu wa Iran, TehranPicha: Atta Kenare/AFP/Getty Images

Mashambulizi hayo yameyalenga pia maeneo mengine ya Tehran likiwemo Baraza la Usalama wa Taifa linaloongozwa na Katibu Mkuu Ali Larijani.

Kulingana na jeshi hilo Jengo jingine lililoshambuliwa ni ni Baraza la wataalamu linaloundwa na viongozi 88 wa kidini.

Iran yasema itaendelea na mashambulizi makali zaidi

Hayo yanajiri wakati ambapo walinzi wa Mapinduzi wa Iran wameonya kuwa wataendeleza adhabu ya mashambulizi makali zaidi dhidi ya Marekani na Israel.

Marekani na Israel zilianzisha mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Iran Jumamosi ambapo Kiongozi wa juu zaidi wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi waliuwawa. Iran, imejibu mashambulizi hayo kwa kuishambulia Israel na vituo kadhaa vya Marekani vilivyo katika nchi za Ghuba.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW