1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia shule huko Gaza na kuuawa watu 30

27 Julai 2024

Wapalestina 30 wameuawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa kufuatia shambulizi la Israel katika shule moja huko Deir al Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Uharibifu katika nyumba za makazi huko Deir al Balah (Gaza) kufutia mashambulizi ya IsraelPicha: Ashraf Amra/AA/picture alliance

Jeshi la Israel limedai kuwa lilikua likilenga kituo cha Hamas. Hayo yakiarifiwa, shirika la ulinzi wa raia wa Gaza limesema hivi leo kuwa operesheni ya kijeshi ya Israel iliyoanza siku ya Jumatatu katika mji wa Khan Younis imeua takriban watu 170 na kuwajeruhi mamia ya wengine. Idadi ya vifo huko Gaza imefikia watu 39,258.

Soma pia: Vita vyaendelea Gaza, mchakato wa mazungumzo wakwama

Jeshi la Israel limetoa limewaamuru tena wakazi wa mji huo wa kusini wa Khan Younis kuondoka eneo hilo baada ya kuopoa miili ya Waisraeli watano na kuonya kuhusu mashambulizi mapya. Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya Wapalestina 180,000 tayari wamekimbia mapigano eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW