1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia tena Lebanon

20 Septemba 2024

Israel imewashambulia wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon masaa machache baada ya kiongozi wao, Hassan Nasrallah, kuapa kulipiza kisasi mashambulizi ya kieletroniki yaliyouwa watu 37 na kuwajeruhi maelfu ya wengine.

Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Israel nchini Lebanon.
Moshi ukizuka baada ya mashambulizi ya Israel nchini Lebanon.Picha: Ali Hashisho/XInhua/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Lebanon Abdallah Bou Habib amesema shambulio hilo ni la wazi dhidi ya mamlaka na usalama wa Lebanon na kwamba linahatarisha eneo zima kutumbukia katika vita.

Marekani pamoja na mataifa mengine ya kigeni yametoa wito kwa pande zote kujizuwia na kuufanya mzozo huwa kubwa mbaya zaidi.

"Shambulio lolote litakalozidisha hali ya mvutano katika eneo hilo halitasaidia kupunguza mvutano huo. Hakika tunachotaka ni kuona makubaliano ya kusitisha mapigano yanafikiwa. Tunataka kuona mateka wakirejea nyumbani. Tunataka kushuhudia vita vya Gaza vikimalizika." Alisema naibu katibu wa masuala ya habari katika wizara ya ulinzi ya Marekani, Sabrina Singh.

Soma zaidi: Netanyahu aanza ziara nchini Marekani

Hata hivyo, maafisa kadhaa wa Marekani wamesema wanaamini kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas huko Gaza hayawezekani kabla ya Rais Joe Biden kuondoka madarakani mwezi Januari.

Marekani imesema mkataba huo wa amani utasaidia kutuliza hali Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW