Israel yatambua mwili wa mateka uliorejeshwa kutoka Gaza
8 Novemba 2025
Matangazo
Jeshi la Israel limeutambua mwili huo uliorejeshwa jana kuwa wa dereva aliyejitolea wa gari ya wagonjwa, Lior Rudaeff, ambaye aliuawa katika shambulizi la Hamas la Oktoba 7, 2023 lililoanzisha vita vya Gaza.
Rudaeff, Muisraeli mwenye asili ya Argentina alikuwa na umri wa miaka 61 wakati wa shambulio hilo na ni mmoja wa raia watano waliokuwa na silaha aliyeuawa alipokuwa akijaribu kutetea jamii yake ya Nir Yitzhak Kibbutz.
Kundi la Familia za Mateka na Waliopotea la Israel, limepongeza hatua ya kurejeshwa kwa mwili huo na kusema inaleta faraja kwa familia za waathiriwa.