1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatanga kuanzisha mashambulizi magharibi mwa Iran

15 Machi 2026

Jeshi la Israel, linalojulikana kama Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF), linasema limeanzisha wimbi kubwa la mashambulizi katika eneo la magharibi mwa Iran.

Israel Kaskazini mwa Israel 2026 | Mwanajeshi wa Israel anasimama karibu na tanki katika mpaka wa Lebanon
Jeshi la Israeli linasema Iran imerusha makombora kuelekea IsraeliPicha: Amir Levy/Getty Images

Jeshi la Israel limesema Jumapili kwamba limeanzisha mashambulizi mapya dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya Iran katika sehemu ya magharibi ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, mashambulizi hayo ni sehemu ya operesheni kubwa inayolenga kile ilichokiita "miundombinu ya utawala wa Iran." Jeshi hilo limesema pia limeharibu vifaa kadhaa vya kurushia makombora na miundombinu mingine ya kijeshi.

Wakati huo huo, mamlaka za Israel zimeripoti mashambulizi kadhaa ya makombora kutoka Iran usiku kucha hadi Jumapili asubuhi.

Nchi kadhaa za Ghuba zimeripoti pia mashambulizi yanayoendelea ya makombora na ndege zisizo na rubani kutoka Iran.

Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imesema makombora sita ya masafa marefu yaliangushwa juu ya mkoa wa Al Kharj, eneo ambako inakutikana kambi ya jeshi ya Prince Sultan.

Walinzi wa Mapinduzi wa Iran walisema Jumamosi jioni kwamba wamerusha makombora dhidi ya wanajeshi wa Marekani walioko kwenye kisiwa hicho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW