1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yatangaza kusitisha mashambulizi yake Gaza

20 Oktoba 2025

Israel imetangaza Jumapili kusitisha mashambulizi yake ya anga katika Ukanda wa Gaza ambayo kulingana na mamlaka za afya yamesababisha vifo vya watu 45.

Gaza 2025 | Mashambulizi ya Israel huko Gaza yaua watu 45
Mashambulizi ya Israel huko Gaza siku ya Jumapili 19.10.2025Picha: Amir Cohen/REUTERS

Jeshi la Israel lilidai kuwa lilishambulia maeneo kadhaa yanayodhibitiwa na Hamas, baada ya wanamgambo wa kundi hilo la Kipalestina kuwashambulia na kuwaua wanajeshi wake wawili huko Rafah, kusini mwa  Gaza.

Hamas kwa upande wao wanasema Israel inatafuta sababu za kuanzisha tena mapigano. Pande zote mbili zimekuwa zikitupiana lawama kwa kukiuka mpango huo wa kusitisha mapigano uliosimamiwa na rais wa Marekani Donald Trump na uliodumu kwa siku tisa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW