Janga
Israel yatangaza operesheni ya ardhini dhidi ya Hezbollah
16 Machi 2026
Matangazo
Jeshi la Israel limesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kujiimarisha na kujilinda dhidi ya kundi hilo.
Tangazo hilo linafanana na lile lililotolewa mwaka 2024 wakati Israel na Hezbollah walipopigana vita vikubwa nchini Lebanon na mwaka 2023 wakati Jeshi hilo hilo la Israel, lilipoanzisha operesheni ya ardhini dhidi ya Ukanda wa Gaza, kujibu mashambulizi ya kundi jengine la wanamgambo wa kipalestina Kusini mwa Tel Aviv mnamo Oktoba 7.
Tangazo hilo hata hivyo limetolewa saa kadhaa baada ya Israel kushambulia Kusini mwa Beirut, ngome ya Hezbollah iliyo makaazi ya maelfu ya raia wa Lebanon.
Mwanzoni mwa vita vya mahasimu hao wawili Israel ilitoa onyo kwa watu kuondoka huko hali iliyosababisha wakaazi wengi kupoteza makaazi yao.