1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yatanua operesheni ya ardhini Ukanda wa Gaza

28 Oktoba 2023

Israel leo imetanua operesheni yake ya kijeshi ya ardhini huko Ukanda wa Gaza ikituma vifaru na magari ya kivita yakisaidiwa na mashambulizi makali ya anga na mengine kutokea baharini.

Wanajeshi wa Israel
Wanajeshi wa Israel wakielekea mpaka wa nchi hiyo na Ukanda wa Gaza Picha: Dan Kitwood/Getty Images

Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amearifu kuwa vikosi vya ardhini vilivyoanza kutumwa kwa awamu hapo jana bado vipo ndani ya Ukanda wa Gaza.

Picha zilizotolewa na jeshi la Israel zimeonesha pia msururu wa vifaru ukisonga mbele taratibu kwenye maeneo ya wazi ya Gaza hali inayoashiria kuanza kwa operesheni ya ardhini iliyosubiriwa.

Mapema hii leo Israel ilisema imeyashambulia maeneo ya Kundi la Hamas ndani ya ukanda huo ikiyalenga mahandaki na miundombonu mingine ya kundi hilo ililoliorodhesha kuwa la kigaidi. 

Wizara ya Afya huko Ukanda wa Gaza imesema watu 7,700 wameuwawa tangu Israel ilipoanza hujuma zake kujibu shambulizi la Oktoba 7 lililofanywa na kundi la Hamas ndani ya Israel.

Shambulizi hilo liliwauwa watu 1,400 na mamia wengine wamechukuliwa mateka.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW