Israel yatarajiwa kukubali usitishaji vita na Hezbollah
26 Novemba 2024Israeli inaonekana kuwa tayari kupitisha mpango wa Marekani wa kusitisha mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah. Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa Israel.
Soma kwa kina kuhusu makubaliano hayo: Israel na Lebanon zakubali masharti ya kusitisha vita
Baraza la usalama la Israel linatarajiwa kukutana baadaye leo Jumanne ili kujadili na pengine kuidhinisha kwa mpango huo kwenye mkutano unaoongozwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.
Mkataba huo tayari umeidhinishwa mjini Beirut, ambako Naibu spika wa bunge la Lebanon ameliambia shirika la habari la Reuters hapakuwa na vikwazo vizito vilivyosalia vitakavyozuia makubaliano hayo kuanza kutekelezwa, labda Netanyahu abadili mawazo.
Naibu spika wa bunge la Lebanon, Elias Bou Saab amesema mpango huo unawataka wanajeshi wa Israel kuondoka kusini mwa Lebanon na wanajeshi wa Lebanon kupelekwa katika vikosi vyake katika eneo la mpaka, ngome ya Hezbollah ndani ya siku 60.