MigogoroMashariki ya Kati
Israel kukifungua kivuko muhimu cha Rafah
15 Oktoba 2025
Matangazo
Hatua hii ni sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani. Takriban malori 600 yaliyosheheni msaada wa chakula, dawa pamoja na vifaa vinavyohitajika kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na vita, yanatarajiwa kuruhusiwa kuingia Gaza.
Siku ya Jumanne, Israel ilitishia kukifunga kivuko hicho muhimu cha Rafah kinachopakana na nchi ya Misri baada ya kudai kuwa Hamas ilishindwa kuheshimu makubaliano hayo kwa kutokabidhi miili ya mateka waliosalia. Lakini baadaye Hamas waliikabidhi miili ya mateka hao wanne. Mashirika ya misaada yametoa wito wa kuongeza mtiririko wa misaada huko Gaza wakisema kuwa mahitaji ni makubwa mno.