1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yamuua kamanda wa kundi la kijeshi la Fatah

22 Agosti 2024

Jeshi la Israel limethibitisha kumuua kamanda wa kundi la kijeshi la Fatah, Khalil al-Maqdah, likimtuhumu kwa kupanga mashambulizi katika Ukingo wa Magharibi

Vifaru vya jeshi la Israel vikiwa katika uwanja wa vita.
Vifaru vya jeshi la Israel vikiwa katika uwanja wa vita.Picha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa al-Maqdah ameuawa jana Jumatano katika shambulizi la anga katika eneo la Sidon, kusini mwa Lebanon.

Fatah, ambao wana makao yao katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israel na wanahasimiana na Hamas, watawala wa Ukanda wa Gaza, wamethibitisha kifo hicho. 

Soma pia:Israel yamuua afisa mwandamizi wa Fatah

Israel imedai kuwa al-Maqdah ni kaka wa Mounir Maqdah anayeongoza kikosi cha mashahidi cha Al Aqsa, ambacho ni tawi la wapiganaji la chama cha Fatah, na imawatuhumu wote kwa kupanga mashambulizi na kufanya biashara ya magendo ya silaha kwenye eneo linalolikaliwa kimabavu na Israel la Ukingo wa Magharibi.

Jeshi la Israel limesema ndugu hao walikuwa wakishirikiana kwa niaba ya Walinzi wa Mapinduzi wa Iran.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW