Israel yatishia kuushambulia zaidi Ukanda wa Gaza
3 Novemba 2025
Matangazo
Mpaka sasa kundi hilo tayari limewaachia mateka 20 walio hai wa Israel baada ya makubaliano ya usitishaji mapigano baina yao na Israel.
Lakini mchakato wa kuirudisha miili nane iliyosalia umekuwa wa polepole mno. Kundi hilo limekuwa likiachia mwili mmoja mmoja au miwili kila baada ya siku chache.
Maadai ya Hamas ni kwamba haijaweza kuyafikia mabaki yote ya miili kwa sababu yako chini ya vifusi vilivyotokana na mashambulizi ya Israel katika Ukanda huo wa Gaza.
Israel yenyewe tayari imerudisha miili ya Wapalestina 225 iliyokuwa inaizuiliwa nchini mwake bila kutoa maelezo yeyote kuhusu utambulisho wao.