1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa dazeni kadhaa Gaza

8 Januari 2025

Mashambulizi ya anga ya vikosi vya Israel leo Jumatano yamewaua watu 22 katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa madaktari wa Palestina.

Ukanda wa Gaza | Mazishi ya mahanga wa mashambulizi ya Israel
Mashambulizi ya Israel yameua dazeni kadhaa za watu Gaza katika muda wa saa 24.Picha: Hatem Khaled/REUTERS

Madaktari wamesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya Sheikh Radwan, Zeitoun, na Deir Al Balah katikati mwa Gaza. Miongoni mwa waathirika ni watoto, huku familia moja ikieleza huzuni yao baada ya kupoteza mpendwa wao.

Mayson Abu Al Qomsan, ambaye alimpoteza mtoto wa dada yake katika shambulio hilo, amesema: "Dada yangu alikuwa kwenye hema na walimrushia kombora yeye na watoto wake. Kosa lao lilikuwa nini? Naapa hawakuwa na uhusiano na chochote. Walikuwa wanapigwa na baridi, sasa wameuawa na mashambulizi ya Israel. Hili, kwa Mungu, ni dhambi."

Soma pia: Vyanzo: Mashambulizi ya Israel yawaua zaidi ya watu 20 Gaza

Huku mashambulizi yakizidi, juhudi za upatanishi zimeongezwa kasi. Chanzo karibu na mazungumzo hayo kimedokeza kuwa kikao cha hivi karibuni kimeweka mkazo mkubwa ikilinganishwa na vikao vya awali. Marekani inaendelea kushinikiza pande zote kufikia makubaliano ya kusitisha vita ili kumaliza mgogoro huu wa muda mrefu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW