1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaushambulia kwa makombora mji mkuu wa Yemen, Sanaa

19 Desemba 2024

Israel imefanya mashambulizi makali ya anga kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa, unaodhibitiwa na waasi wa Kihouthi na miji ya bandari wa Hodaida, na kusababisha vifo vya watu tisa.

Mashambulizi ya anga ya Israel mjini Sanaa
Maafisa wa zimamoto wakiukabili moto kwenye kituo cha umeme kufuatia mashambulizi ya anga ya Israel mjini SanaaPicha: Khaled Abdullah/REUTERS

Wahouthi wanasemekana walishambulia Israel kwa kombora, hatua inayoongeza mvutano kati ya Israel na waasi hao wanaoungwa mkono na Iran.

Soma pia: Israel imesema imefanikiwa kulizuia kombora kutoka Yemen

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, alilaani mashambulizi hayo na kuyaita ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Televisheni ya al-Masirah ya waasi wa Houthi iliripoti kuwa mashambulizi yalilenga vituo vya nishati na bandari, ikiwemo termino ya mafuta ya Ras Isa na bandari ya Salif, ambako watu saba waliuawa.

Israel ilidai mashambulizi hayo yalilenga kuzima shughuli za kijeshi za Wahouthi, ikiwemo usafirishaji wa silaha kutoka Iran, na kusema itaendelea kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Houthi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW