SiasaIsrael
Israel yawapiga risasi wanaodaiwa wapiganaji 3 wa Palestina
25 Julai 2023Matangazo
Vikosi vya usalama vya Israel vimesema vilijibu mashambulizi ya risasi kutoka kwa wapiganaji wa Kipalestina waliowakuwamo kwenye gari moja katika mji wa Nablus, ambao ndio mji mkuu wa kibiashara wa eneo hilo na kiini cha mashambulizi ya hivi karibuni ya jeshi la Israeli.
Vyombo vya habari vya Palestina vimeelezea mauaji hayo ya Israel kuwa tukio la kuvizia kufuatia jaribio la wanamgambo hao wa Palestina kushambulia vikosi vya Israel karibu na makaazi ya Wayahudi yaliyoko karibu na Nablus. Jeshi la Israel limesema limekamata bunduki tatu aina ya M-16 na silaha nyengine kwenye gari hilo.