1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawasili Cairo kwa mazungumzo ya vita vya Gaza

3 Agosti 2024

Ujumbe wa Israel umewasili mjini Cairo leo kushiriki mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja juu ya vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza katikati ya kiwingu cha kutanuka kwa mzozo wa kijeshi kwenye kanda ya Mashariki ya Kati.

David Barnea
Ujumbe huo wa Israel unamjumuisha Mkuu wa Shirika la Ujasusi, Mossad, David BarneaPicha: Amir Cohen/REUTERS

Ujumbe wa Israel umewasili mjini Cairo kushiriki mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja juu ya vita vinavyoendelea Ukanda wa Gaza katikati ya kiwingu cha kutanuka kwa mzozo wa kijeshi kwenye kanda ya Mashariki ya Kati. 

Ujumbe huo wa Israel unamjumuisha Mkuu wa Shirika la Ujasusi, Mossad,David Barnea na kiongizi wa idara ya usalama wa taifa, Shin Bet, Ronen Bar. 

Duru zinasema awamu hiyo ya sasa ya mazungumzo itajikita katika suala la kuachiwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa na kundi la Hamas pamoja na hatma ya usalama kwenye eneo la mpaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza. 

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati hofu imetanda ya kusambaa kwa mzozo wa kijeshi kwenye kanda hiyo kufuatia kuuawa kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh na shambulizi la Israel nchini Lebanon lililomuua kamanda wa ngazi ya juu wa Hezbollah. Haniyeh aliuwawa mjini Tehran na Iran imesema shambulio hilo lilifanywa na Israe

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW