SiasaIsrael
Israel yaendeleza mashambulizi kusini mwa Gaza
19 Januari 2024Matangazo
Watu walioshuhudia mashambulizi hayo wamesema milio ya risasi na mashambulizi ya anga yalisikika mapema asubuhi huko Khan Younis, ambako Israel imesema wanamgambo wengi na viongozi wa kundi la Hamas wanajificha.
Shirika la Hilal Nyekundu la Palestina limeripoti kuhusu mashambulizi makali ya makombora karibu na hospitali ya Al-Amal.
Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza, imesema watu 77 wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano ya usiku kucha.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesisitiza kwamba vita dhidi ya Hamas vitachukua muda mrefu.