1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yazidi kushinikizwa isiivamie Rafah

16 Februari 2024

Marekani imeitolea tena wito Israel wa kutofanya mashambulizi ya kiwango kikubwa katika mji wa Rafah ulioko kusini mwa Gaza, ambako karibu Wapalestina milioni 1.5 wamekimbilia kutafuta hifadhi.

Watoto wa Kipalestina wakiandamana kupinga vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.
Watoto wa Kipalestina wakiandamana kupinga vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza.Picha: Ahmad Hasaballah/Getty Images

Ikulu ya White House, ilisema Rais Joe Biden alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jioni ya Alhamis (Februari 15) na kumtaka kutofanya mashambulizi mjini Rafah bila ya mpango wa kuhakikisha usalama wa raia katika eneo hilo.

Ujerumani, Uingereza, Australia, Canada na New Zealand pia zimeitaka Israel kutofanya mashambulizi ya ardhini katika mji huo wa Rafah.

Soma zaidi: Viongozi wa dunia waisihi Israel kuacha operesheni ya Rafah

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak imesema kwamba kiongozi huyo amemwambia Netanyahu kwa njia ya simu kwamba Uingereza ina wasiwasi mkubwa kuhusu uwezekano wa kuzuka janga la kibinaadamu kutokana na uvamizi wa kijeshi mjini Rafah.

Hata hivyo, Netanyahu amesisitiza kuwa ataendelea na operesheni katika mji huo wenye idadi kubwa ya watu hadi atakapopata ushindi kamili dhidi ya kundi la wanamgambo wa Hamas.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW