1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yazidisha mashambulizi kaskazini na kusini mwa Gaza

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Mashambulizi makali ya jeshi la Israel, yameripotiwa leo Jumatatu, katika mji wa Jabalia, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Hamas-Israel-Vita | Wanajeshi wa Israel wakiwa Ukanda wa Gaza
Wanajeshi wa Israel wakifanya mashambulizi Ukanda wa Gaza.Picha: Israel Defense Forces/REUTERS

Huku wakaazi na kundi la Hamas wakisema kuwa vifaru vya kijeshi, na wanajeshi wa Israel, walivuka mpaka na kupiga kambi karibu na viunga vya Rafah, kusini mwa Gaza.

Taarifa zimesema, huko Jabalia, vifaru vya jeshi la Israel vilikuwa vikisonga mbele, kuelekea kambi ya wakimbizi ya mji huo. Wakaazi na madaktari walisema watu kadhaa waliuawa, na wengine wamejeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi ya anga, kwenye kambi hiyo, usiku kucha.

Kulingana na wizara ya Afya ya Gaza inayoongozwa na kundi la Hamas, idadi ya vifo katika operesheni ya jeshi la Israel kwenye ukanda huo imefikia zaidi ya watu 35,000.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW