1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yazidisha mashambulizi katika Ukanda wa Gaza

17 Julai 2024

Jeshi la Israel limeendeleza mashambulizi katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya Wapalestina tisa wakati vifaru vya jeshi vikisonga taratibu kwenye mji wa kusini wa Rafah.

Israel kuendelea kuishambulia Gaza kwa lengo la kuwaangamiza kabisa wanamgambo wa Hamas
Isreal yazidisha mashambulizi katika Ukanda wa GazaPicha: Tsafrir Abayov/AP/picture alliance

Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wanaendelea kwa usahihi na operesheni zake kwa kutumia taarifa za kijasusi katika eneo la Rafah ambako wanadai kuondoa kile walichokiita "kiini cha ugaidi."

Wizara ya Ulinzi wa Israel, imesema waziri wake Yoav Gallant amemwambia mwenzake wa Marekani  Lloyd Austin kwamba operesheni za kijeshi katika Ukanda wa Gaza zimeweka mazingira ya kuwezesha kufikiwa makubaliano ya kubadilishana wafungwa.

Israel yaendeleza mashambulizi Gaza licha ya ukosoaji wa Marekani

Juhudi za kidiplomasia za wapatanishi wa mataifa ya kiarabu zinazoungwa mkono na Marekani zinaendelea lakini pande hasimu zinashinikiza masharti tofauti.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW