1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul: Idadi ya waliofariki imeongezeka

18 Novemba 2003

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mashambulio mawili ya kujitolea mhanga katika masinagogi mawili mjini Istanbul, Uturuki imeongezeka na kufikia 25. Shirika la Habari la Uturuki, ANADOLU, limeripoti kuwa mtu mwingine aliyejeruhiwa amefariki hospitalini. Mwanamke aliyekuwa akitafutwa amepatikana amefariki katika mabaki ya Sinagogi la Beth-Israeli. Watu wapatao 300 wamejeruhiwa wakati wa mashambulio hayo yaliyofanywa Jumamosi iliyopita. Shirika la Habari la ANADOLU limeripoti kuwa Polisi wa Uturuki wamewatambua wauaji wawili wa kujitolea mhanga. Wanaume hao wawili ni Waislamu wa Kituruki wenye itikadi kali. Maiti zao zitafanyiwa uchunguzi kabla ya kuzikwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW