1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Majirani wa Iraq wakutana Istanbul

30 Aprili 2005

Uturuki imetoa wito kwa nchi jirani za Iraq kuiunga mkono serikali mpya mjini Baghdad,ili kuleta utulivu na umoja nchini humo.Waziri mkuu Tayyip Erdogan wa Uturuki ameuambia mkutano wa mawaziri wa kigeni na maofisa wengine mjini Istanbul,kuwa utulivu nchini Iraq ni jambo linaloihusu kanda nzima.Vile vile amesema angependa kuona mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Umoja wa nchi za Kiarabu,yakijishughulisha zaidi kwa vitendo nchini Iraq.Mbali na wajumbe wa nchi sita zinazopakana na Iraq ambazo ni Uturuki,Iran,Kuwait,Saudi Arabia,Jordan na Syria,mkutano huo umehudhuriwa vile vile na wajumbe kutoka Misri na Bahrain.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW