1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Mripuko mwingine wa bomu umeua watu 2

28 Agosti 2006

Watu 2 wameuawa na 6 wengine wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea kati kati ya mji wa Antalya kusini mwa Uturuki.Mripuko huo unafuata miripuko mingine ya bomu iliyotokea katika mji wa pwani wa Marmaris na Istanbul chini ya saa 24 zilizopita.Katika miripuko hiyo ya bomu watu 27 walijeruhiwa.Katika shambulio jingine bomu lililofichwa ndani ya barua,liliripuka mji mkuu wa biashara,Istanbul na kuwajeruhi watu 6.Maafisa wa polisi wanaamini kuwa wanamgambo wa Kikurd wamehusika na shambulio hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW