1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Istanbul, Uturuki. Papa amaliza ziara yake Uturuki.

1 Desemba 2006

Papa Benedict 16 ameondoka nchini Uturuki mwishoni mwa ziara yake katika taifa la Kiislamu. Hapo mapema , kiongozi huyo wa kanisa Katoliki aliongoza misa mjini Istanbul kwa waumini wa jamii ndogo ya Wakatoliki.

Kabla ya misa hiyo Benedict aliwaachilia njiwa wanne weupe hewani , ikiwa ni ishara ya amani.

Wakati wa hotuba yake, kiongozi huyo wa kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka 79 amesema kuwa Vatican haina nia ya kulazimisha chochote kwa yeyote, na kwamba kanisa linatumai tu kuishi katika amani na uhuru.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW