1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL: Waasi wa Kikurd wapambana na walinzi

3 Aprili 2005

Watu 3 wameuawa katika mapambano yaliozuka kati ya waasi wa Kikurd na askari jeshi,kusini-mashariki mwa Uturuki.Afisa wa kijeshi amesema waasi 2 na mlinzi 1 wa kijijini waliuawa baada ya waasi kutoka chama cha PKK kukishambulia kikundi cha wanajeshi.Kiasi ya walinzi 50,000 katika vijiji,wakiungwa mkono na serikali hupiga doria katika eneo ambalo waasi wanadai kuwa ni ardhi yao ya kikabila.Tangu wanamgambo wa Kikurd kuanzisha mapigano yao mwaka 1984,zaidi ya watu 30,000 wameuawa,wengi wao wakiwa Wakurdi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW