ISTANBUL:Helikopta za Uturuki zashambulia vijiji vya Irak
13 Novemba 2007Matangazo
Habari zinasema helikopta za Uturuki zimeshambulia vijjiji vya ndani ya Irak ambavyo vimehamwa. Idara za serikali za Irak zimesema hiyo ni mara ya kwanza kwa ndege za Uturuki kufanya mashambulio tokea mvutano wa mpakani na kaskazini mwa Irak uanze.
Msemaji wa majeshi ya Uturuki ameeleza kuwa mashambulio hayo yalifanyika katika vijiji vilivyopo karibu na mji wa Zhaku uliopo ndani ya Irak
Wakati huo huo wizara ya ulinzi ya Uturuki imearifu kuwa askari wake wanne waliuawa katika mapambano na wapiganaji wa kikurdi wa PKK kusini mashariki mwa Uturuki.