1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISTANBUL:Watu watano wauawa mjini Istanbul.

4 Agosti 2005

Polisi nchini Uturuki wameeleza watu wawili wameuawa na wengine wanaofikia watano wamejeruhia,baada ya kutokea mripuko katika mji wa Istanbul.Mripuko huo ulitokea katika wilaya ya Pendik.

Kumekuwa na ripoti za kukanganya namna mripuko huo ulivyotokea.Kituo cha habari cha televisheni cha CNN-Turk,kimesema mripuko huo umetokea ndani ya gari lililokuwa katika mwendo,wakati watu walioshuhudia wamekieleza kituo cha televisheni cha Star bomu lililoripuka lilikuwa limefichwa ndani ya pipa la taka.

Uturuki imekumbwa na mfululizo wa miripuko ya mabomu katika miezi ya hivi karibuni na shutuma nyingi zikielekezwa kwa wanamgambo wa Kikurdi wanaotaka kujitenga.

Mwezi uliopita watu watano waliuawa,baada ya basi dogo kushambuliwa kwa bomu katika eneo mashuhuri la mapumziko la Kusadasi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW