1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Itachukua miezi mitatu kuachiwa huru Wamarekani huko Iran.

21 Agosti 2023

Mchakato wa kuachiwa huru raia wa Marekani wanaoshikiliwa katika jela za Iran utachukuwa kipindi cha hadi miezi miwili kutekelezwa.

Iran | Eingang des Evin prison in Tehran | Archivbild 2022
Picha: WANA NEWS AGENCY/File Photo/REUTERS

Hayo yameelezwa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Nasser Kanaani, katika mkutano na waandishi wa habari.Mwanzoni mwa mwezi huu, serikali ya Iran na Marekani zilifikia makubaliano ya kuachiwa huru raia watano wa Marekani wanaozuiliwa Iran huku Marekani ikitakiwa kuziachia dola bilioni 6, fedha za Iran zinazozuiliwa katika akaunti nchini Korea Kusini. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Korea Kusini, fedha hizo zilihamishwa na kupelekwa katika benki kuu ya Uswizi wiki iliyopita kwa ajili ya kuwa tayari kuhamishiwa Iran baada ya mchakato huo wa kubadilishana kukamilika.Iran imesema  Marekani pia itatakiwa kuwaachia huru baadhi ya Wairani inaowazuilia katika jela zake. Iran imeruhusu wafungwa wanne wa Kimarekani waliokuwa wakishikiliwa katika jela ya Evin mjini Tehran, wawekwe katika kifungo cha nyumbani katika makaazi maalum nchini humo.