1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia imelitambua Baraza la Waasi nchini Libya

Admin.WagnerD4 Aprili 2011

Italia leo imelitambua Baraza la Mpito la Waasi nchini Libya kama chombo kinachowakilisha Umma wa nchi hiyo na kuahidi kusaida kufufua uchumi pamoja na ujenzi mpya wa mji mkuu wa waasi hao wa Bengazi. Sudi Mnette anaari

Mwakilishi wa Waasi Ali al-Essawi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki Franco FrattiniPicha: dapd

Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mahusiano ya Nje wa Baraza hilo,Ali al-Isawi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia,Franco Frattini amesema nchi yake imeamua kulitambua baraza hilo la mpito.

Mpaka sasa nchi za Ufaransa na Qatar zimekwishalitambua baraza hilo kama chombo kinachowawakilisha Walibya.

Akizungumza kutoka Benghazi baada ya kusikia habari hiyo kupitia vyombo vya habari,Msemaji wa Baraza la Mpito la Waasi,Mustafa Gheriani amesema hiyo ni hatua kubwa kwao.

Frattini amesema watatuma wataalam kwa lengo la kustawisha uchumi pamoja na ujenzi wa mji wa Benghazi ambao umeharibiwa vibaya kutokana na vita inayoendelea sasa.

Aidha Italia imeahirisha mazungumzo ya kutafuta amani yanayoratibiwa na Gadhafi kupitia Naibi Waziri wake wa Mambo ya Nje,Abdelati Laabidi kutokana na Gadhafi kutonesha nia ya kuondoka madarakani.

Frattini amesema kutokana na taarifa waliyonayo kutoka Ugiriki kwamba Gadhafi atasimamisha mapigano lakini hakuonesha nia ya kuondoka nchini humo kwa shabaha ya kuacha uwanja mpya wa demokrasia.

Uingereza imesema haiwezi kuzua jitihada yeyote inayofanywa na Kiongozi wa Libya Muammar Gadhafi katika kufanikisha utatuzi wa mgogoro nchini humo wakati huu ambapo ujumbe wa kiongozi huyo ukitembea katika mji kadhaa kwa lengo la kutafuta suluhu.

Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameroon,amesema msimamo wa nchi hiyo uko wazi kabisa,nao ni kusimamisha mapigano na kumaliza kabisa vurugu nchini humo.

Akiwasilisha taarifa hiyo kwa Waandishi wa habari amesema kumekuwa na taarifa nyingi ambazo zimesikika kwa namna tofauti kwa hivyo jambo hilo hawana kipingamizi nalo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya,Abdelati Laabidi hivi sasa yupo Uturuki na baade Malta akitokea nchini Ugiriki ambapo kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo,Dimitris Droutsas anasema anatafuta suluhu ya mgogoro.

Wapiganaji nchini LibyaPicha: dapd

Wakati huo huo,mapigano nchini Libya yamekuwa yakiendelea kwa namna tofauti ambapo leo hii,vikosi vitiifu kwa Kanali Gadhafi vimerifyatua mabomu katika mji unaoshikiliwa na Waasi wa Misrata.

Akizungumza na Shirika la Habari-Reuters Msemaji wa Upande wa Upinzani amesema kitendo hicho kimeanza mapema asubuhi na kuongeza kwamba na kwamba milipuko ilielekezwa kwa wakazi.

Amekiita kitendo hicho kuwa cha kigaidi na ingawa hakueleza idadi ya watu waliyoathirika na miripuko hiyo.

Mwandishi:Sudi Mnette/rtr

Mhariri:Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi

Gundua zaidi

Onesha taarifa zaidi