1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia kuipatia Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga na silaha

4 Juni 2024

Serikali ya Ukraine imesema Italia itaipatia nchi hiyo mfumo mwingine wa ulinzi wa anga pamoja na silaha katika hatua ya kuisaidia Kyiv kukabiliana na mashambulizi ya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Gints Ivuskans/AFP

Rais Volodymyr Zelensky amesema Ukraine inahitaji mifumo mingine saba kama hiyo ikiwa ni pamoja na miwili ambayo itasaidia kulinda eneo la mashariki linaloshambuliwa zaidi la Kharkiv.

Soma pia:Scholz: Hakuna hatari Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa silaha za Ujerumani

Hayo yakiripotiwa, Kansela wa Ujerumani Olaf scholz amesema haoni hatari yoyote kuhusiana na kuikubalia Ukraine kutumia silaha inazopewa na Ujerumani kushambulia ndani ya Urusi na kwamba hatua hiyo haitopelekea kutanuka kwa mzozo huo.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW