Italia na Libya zakubaliana kudhibiti wahamiaji
30 Desemba 2007Matangazo
TRIPOLI.Italia na Libya zimekubaliana kufanya doria ya pamoja katika pwani ya bahari ya Mediterrania kuzuia wahamiaji haramu wanaotoka afrika kwenda Ulaya.
Chini ya makubaliano hayo, Italia itatoa boti sita za doria kuwasaidia maafisa wa nchi hizo mbili katika harakati hizo.
Kila mwaka maelfu ya wahamiaji haramu wa afrika wanajaribu kuingia Ulaya kwa kutumia njia hatari za baharini.
Waziri wa mambo ya ndani wa Italia Giuliano Amato amesema kuwa mpango huo utaokoa maisha maisha ya watu na kuvunjilia mbali makundi ya kihalifu.