1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaItaly

Italia yaidhinisha $ bilioni 2.2 kwa waathiriwa wa mafuriko

24 Mei 2023

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amesema hii leo kuwa serikali yake imeidhinisha kitita cha msaada wa dharura.

Italien I Überschwemmungsgebiet Emilia-Romagna
Picha: Palazzo Chigi press office/AFP

Chenye thamani ya dola bilioni 2.2 ili kuyasaidia maeneo yaliyokumbwa na mafuriko katika eneo la Kaskazini la Emilia-Romagna.

Soma pia: Watu 30 hawajulikani walipo baada ya mashua kuzama

Karibu wiki moja baada ya janga hilo, watu wapatao 23,000 wamesalia bila makazi huku baadhi ya miji ikiwa bado inakabiliwa na mafuriko yaliyoharibu pia maelfu ekari za mashamba yenye rutuba.

Meloni amesema msaada huo unajumuisha gharama za shughuli za dharura pamoja na kusitisha kwa muda michango katika fuko la kijamii na kodi mbalimbali kwa kaya na makampuni.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW