1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia yaitisha mkutano kukabiliana na wahamiaji

Sylvia Mwehozi
23 Julai 2023

Italia imezialika nchi za Mediterania kuhudhuria mkutano wa kimataifa unaolenga kurefusha mkataba wake na Tunisia wa kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaowasili katika pwani za Ulaya unaofanyika leo Jumapili.

Italia, Tunisia, Umoja wa Ulaya
Viongozi wa Italia, Tunisia, Umoja wa UlayaPicha: Freek van den Bergh/ANP/picture alliance

Italia imezialika nchi za Mediterania kuhudhuria mkutano wa kimataifa unaolenga kurefusha mkataba wake na Tunisiawa kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaowasili katika pwani za Ulaya unaofanyika leo Jumapili.

Waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, anatarajia kukutana na viongozi wa Umoja wa Ulaya na taasisi za fedha za kimataifa mjini Roma katika kuurefusha mkataba huo unaoungwa mkono na Umoja wa Ulaya.

Licha ya kuwa, orodha ya viongozi watakaohudhuria mkutano huo haijawekwa wazi, Meloni amethibitisha uwepo wa Rais wa Tunisia Kais Saied. Mawaziri wakuu wa Misri na Malta pia wamesema watahudhuria.

Takwimu za Italia zinaonesha kuwa tangu mwezi Januari mwaka huu, wahamiaji 80,000 walifika Pwani ya Italia ikilinganishwa na 33,000 waliowasili nchini humo kwa kipindi kama hicho mwaka uliopita. Wengi wanatoka Tunisia na Libya.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW