1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia yapitisha kanuni mpya kuwakabili wahamiaji

19 Septemba 2023

Italia imeidhinisha kanuni mpya zinazorefusha muda wa wahamiaji wasio na vibali kubakia chini ya vizuizi wakati wakisubiri kurejeshwa kwenye mataifa wayoyakimbia.

Wahamiaji wengi kutoka Afrika Kaskazini wakiwasili kisiwani Silicy, Italia
Wahamiaji wengi kutoka Afrika Kaskazini wakiwasili kisiwani Silicy, Italia Picha: Salvatore Cavalli/AP Photo/picture alliance

Baraza la Mawaziri la nchi hiyo limepitisha uamuzi huo jana jioni ikiwa ni hatua ya hivi karibuni kabisa ya kukabiliana na wimbi la wahamiaji wanaongia Italia, wengi kutoka barani Afrika.

Waziri Mkuu anayegemea siasa za mrengo mkali wa kulia, Giorgio Meloni, amesema uamuzi uliopitishwa utaruhusu wahamiaji kuwekwa kizuizini kwa muda wa kati ya siku 135 na usiozidi miezi 18 kabla ya kurejeshwa walikotoka.

Amesema serikali yake inataka kutuma ujumbe kote barani Afrika kwamba Italia itawachukulia hatua wote watakaovunja sheria kwa kujaribu kuingia nchini humo kwa njia za magendo.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya idadi kubwa ya wahamiajikuingia kwenye kisiwa cha Lampedusa ndani ya wiki chache zilizopita wakitokea kaskazini mwa Afrika.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW