1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia yatangaza hali ya hatari kufuatia mafuriko

21 Septemba 2024

Italia imetangaza hali ya hatari kufuatia mafuriko makubwa katika mikoa yake miwili ya Emilia-Romagna na Marche iliyopo kazkazini mwa nchi hiyo. Hali hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Giorgia Meloni

Italia | Giorgia Meloni
Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni ametangaza hali ya hatari katika mikoa yake miwili kufuatia mafurikoPicha: Matteo Bazzi/ZUMA/picture alliance

Italia imetangaza hali ya hatari leo Jumamosi kufuatia mafuriko makubwa katika mikoa yake miwili ya Emilia-Romagna  na Marche iliyopo kazkazini mwa nchi hiyo. Hali hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Giorgia Meloni na kusema kwamba dola milioni 22 zinahitajika haraka kama msaada wa dharura.

Mvua kubwa imesababisha barabara nyingi kujaa maji katika mikoa hiyo miwili, zaidi ya watu 2,500 wamelazimika kuyakimbia makaazi yao. Miji ya pwani ya Bologna, Modena na Ravenna ni miongoni mwa miji iliyokubwa na kadhia hiyo.

Soma zaidi. Maelfu ya watu wahamishwa Italia kufuatia Kimbunga Boris

Wakati huo huo, kumekuwepo na kutupiana maneno ya lawama kati ya serikali mjini Roma na
serikali za mikoa ya maeneo yaliyokumbwa na mafuriko. Nello Musumeci,Waziri wa ulinzi kutoka serikali hiyo ya mrengo wa kulia alimshutumu kiongozi wa mji wa  Emilia-Romagna kutoka chama cha social-demokratic kwa kutotumia pesa ambazo tayari zilikwishatolewa kwenye mji huo.

Kwa upande wao Social-Democrats walizijibu tuhuma za waziri huyu na kusema kwamba hizo ni njama kuelekea uchaguzi katika jimbo hilo utakaofanyika hapo mwezi Novemba.