Italia yatuma mawaziri Afrika kupata mikataba ya nishati
20 Aprili 2022Matangazo
Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi analenga kuyatumia mataifa mawili ya Angola na Jamhuri ya Congo kama wasambazaji mbadala wa nishati ya Urusi inayofikia asilimia 45 ya gesi yote inayotumika nchini Italia.
Serikali ya Draghi imewatuma waziri wa mambo ya kigeni, Luigi Di Maio, na mwenzake wa Ikolojia, Roberto Cingolani, kwenda mjini Luanda leo Jumatano na baadaye mjini Brazzaville kujadili uwezekano wa kununua nishati kutoka Angola na Jamhuri ya Congo.
Italia, ambayo imeapa kumaliza utegemezi wa nishati ya Urusi, tayari imetia saini mikataba ya kununua gesi kutoka Algeria na Misri na inapanga pia kufanya mazungumzo ya kununua gesi nchini Msumbuji mnamo mwezi Mei.
chanzo: ap