1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jürgen Klopp kuondoka Liverpool

26 Januari 2024

Klabu ya Liverpool inayoshiriki Ligi ya Premier ya England, imetangaza kwamba kocha wake, Jurgen Klopp, ameamua kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

London | Jürgen Klopp,  Liverpool
Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp, kuondoka mwishoni mwa msimu.Picha: CSM/ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Makocha wasaidizi, Pepijn Linjders na Peter Krawietz, pia wataondoka.

Klopp ameufahamisha uongozi wa klabu hiyo kwamba ataacha kuinoa Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kuhitimisha miaka minane na nusu na miamba hao wa Anfield.

Soma zaidi: Klopp azima rekodi ya Man City kutofungwa

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 56 ameiambia tovuti ya Liverpool kuwa, anapenda kila kitu kuhusu klabu hiyo na ana uhakika uamuzi wake ni sahihi.

Amesema ameamua kuondoka kwa sababu ya hana nguvu tena za kuendelea kutekeleza majukumu yake 

Klopp alijiunga na Liverpool Oktoba mwaka 2015 na ameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Premier, Kombe la Dunia ngazi ya Klabu, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Super Cup pamoja na Ngao ya Jamii.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW