1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

240210 Deutsche Literatur

Abdu Said Mtullya25 Februari 2010


Kuna  taasisi  kadhaa  nchini Ujerumani  zinazoshughulikia uenezaji  wa  fasihi  ya kijerumani duniani.Na muhimu  kati  ya taasisi   hizo ni chuo  cha  Goethe.

Katika muda  wa  miaka mingi taasisi hiyo  imesimamia tafsiri za vitabu karibu  alfu  tano  kutoka  nyanja  mbalimbali  za fasihi.

Ujerumani  imebarikiwa  kuwa  na  waandishi  mashuhuri  wa  riwaya, vitabu vya  sayansi na  vitabu  vya  fasihi  ya watoto.

Bertold  Brecht  ni miongoni  mwa waandishi  hao mashuhuri katika tanzu  ya tamthilia.

Sabine  Erlenwein  anaeshughulikia  kazi  za tafsiri  ya  vitabu kwenye   chuo  cha  Goethe  anasema wapo waandishi  ambao hawawezi kupitwa  kama  vile Günther  Grass  lakini amesema pana orodha ndefu  ya  waandishi wa zama za leo.

Miongoni mwa vitabu  vilivyotafsiriwa ni vile vya  Daniel Kelhmann , mwandishi   wa  riwaya maaruf  inayoitwa "kipimo cha  dunia"-  Kazi za  mwandishi  huyo  zimetafsiriwa  katika  lugha   41 .

Erlenwein  anaeshughulikia  tafsiri hizo amefuatilia  kwa  muda  wa miaka  ya hivi karibuni  jinsi fasihi  ya  kijerumani  inavyorejea  tena katika medani  ya  kimataifa  hasa kutokana  na  kuanzishwa   kwa tuzo  ya  uandishi wa  vitabu ambayo  inatolewa   tokea  mwaka wa 2005.

Rika jipya  la waandishi  limejijenga   nchini  Ujerumani.

 Miongoni mwa wa waandishi hao ni Sasa Stanisic  alieandika kitabu maaruf  juu   ya  wakimbizi  wa  vita vya Bosnia.

Vitabu vyake vinauzwa kwa  leseni  katika nchi  20  .

Juu ya  kurejea  kwa fasihi  ya  kijerumani  katika medani ya kimataifa msimamizi  wa  kazi  za tafsiri kwenye  chuo  cha  Goethe bibi Sabine Erlenwein  amesema fasihi   hiyo imefana katika  Ulaya ya kati na ya mashariki.

 Hatahivyo  ameelaza  kwamba  fasihi   hiyo  inakabiliwa na ushindani  mkubwa  katika  nchi  ambapo lugha  ya  kiingereza inatumika.

Taasisi  ya  Goethe inatafsiri  vitabu  kati   ya 250  na  300 kila mwaka,  na  kwa  ajili hiyo  kitengo  cha  ufasiri vitabu  kinapata kiasi  cha Euro  laki  tano  hadi  sita  kila mwaka.

Lakini  chuo cha  Goethe kina   mustakabali  mzuri  kutokana  na waandishi wake  wa   kisasa.

Wasomaji  vitabu  duniani  kote wana uchu  wa kusoma  vitabu  vya waandishi    wa  kijerumani.

Mwandishi/Cordsen  Knut/ZA

Imetafsiriwa  na  Mtullya Abdu/

Mhariri/Abdul-Rahman,Mohammed