1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolsonaro mbaroni kabla ya kuanza kifungo cha miaka 27 jela

22 Novemba 2025

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro amekamatwa na polisi Jumamosi siku kadhaa kabla ya kuanza kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kwa kosa la kuongoza jaribio la kuipindua serikali.

Jair Bolsonaro anakabiliwa na kifungo cha miaka 27 jela
Rais wa zamani wa Brazil Jair BolsonaroPicha: Evaristo Sa/AFP

Jaji Alexandre de Moraes wa Mahakama Kuu ya Brazil amesema Bolsonaro amekamatwa kwasababu ya hatari iliyosababishwa na wafuasi wake kwa kuwazuia polisi waliokuwa wakimfuatilia.

Amebainisha pia kuwa kuna ushahidi wa kujaribu kukihujumu kifaa cha kufuatilia mwenendo wa Bolsonaro alichokuwa amefungwa mguuni. Mwanasheria wa Rais huyo wa zamani wa Brazil, Celso Vilardi amethibitisha kukamatwa kwa mteja wake Jumamosi asubuhi.

Shutuma za jaribio la mapinduzi na kuchochea uasi

Bolsonaro na washirika wake kadhaa walihukumiwa na mahakama hiyo kwa kujaribu kuipindua demokrasia ya Brazil baada ya kushindwa na Rais Luiz Inácio Lula da Silva kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Mapinduzi aliyoyapanga yalijumuisha mipango ya kutaka kumuua Lula na kuchochea uasi mwanzoni mwa mwaka 2023. Alikutwa pia na hatia ya kuongoza genge la uhalifu na kujaribu kuuondoa utawala wa sheria unaofuata demokrasia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW