1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBrazil

Jaji wa Brazil aamuru kufungwa kwa mtandao wa X nchini humo

31 Agosti 2024

Jaji wa Mahakama ya Juu wa Brazil ameamuru hapo jana kufungwa kwa mtandao wa kijamii wa X ( zamani Twitter) nchini humo.

Bendera ya Brazil na nembo ya mtandao wa X (zamani Twitter)
Bendera ya Brazil na nembo ya mtandao wa X (zamani Twitter)Picha: Andre M. Chang/ZUMA Press Wire/picture alliance

Uamuzi huo unajiri baada ya X kushindwa kutii amri ya kumteua mwakilishi mpya wa kampuni hiyo. Sheria ya Brazili inazitaka kampuni zote zinazomiliki mitandao ya kijamii kuwa na mwakilishi wa kisheria katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Mapema mwezi huu, mtandao wa X ulimuondoa mwakilishi wake nchini Brazil baada ya Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil Alexandre de Moraes kutishia kumkamata.

Soma pia: Elon Musk kushitakiwa Brazil

Kwa wiki kadhaa sasa, Jaji Moraes na mmiliki wa X Elon Musk wamekuwa kwenye mvutano juu ya masuala ya uhuru wa kujieleza, akaunti zenye itikali kali za mrengo wa kulia pamoja na habari potofu.