1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Korea mbili zakutana tena Indonesia

23 Aprili 2005

Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini zimejadiliana juu ya mazungumzo yaliokwama kuhusu miradi ya kinuklia ya Pyongyang,lakini hakuna maendeleo yaliopatikana.Huu ni mkutano wa pili wa aina hiyo,tangu nchi hizo kukutana kwa mara ya mwanzo miaka 5 ya nyuma.Wajumbe wa nchi hizo mbili safari hii wamekutana mji mkuu wa Indonesia,Jakarta kando ya mkutano wa kilele wa nchi za Asia na Afrika.Inasemekana kuwa wajumbe hao wamekubaliana kuwa mazungumzo yaliokwama yanapaswa kuanzishwa tena.Korea ya Kaskazini ilivunja mawasiliano rasmi na Korea ya Kusini Julai mwaka jana baada ya Seoul kuwasafirisha kwa ndege kutoka Vitenam,raia 468 wa Korea ya Kaskazini waliotoroka,hatua iliyoihamakisha serikali ya Pyongyang.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW