1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA: Mkakati wa kuimarisha ushirikiano kati ya Asia na Afrika

23 Aprili 2005

Nchi za Asia na Afrika,zimekubali kuanzisha uhusiano mpya wa kiuchumi na kisiasa.Tangazo hilo limetolewa kwenye mkutano wa viongozi wa nchi za Asia na Afrika katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia katika hotuba yake ya kuufunga mkutano wa siku mbili amesema,tangazo la mkakati wa ushirikiano huo kati ya nchi za Asia na Afrika ni tukio muhimu.Na rais Thabo Mbeki wa Afrika ya Kusini alieuongoza mkutano huo pamoja na Yudhoyono,amesema mamilioni ya wananchi wao wanataraji kuona vitendo halisi.Kwa wakati huo huo akaonya kuwa kazi ngumu ya kutekeleza makubaliano yao,inawangojea viongozi hao.