1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA : Mkutano wa Viongozi Asia na Afrika kufanyika Indonesia

19 Aprili 2005

Viongozi wa Kiafrika walioalikwa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wiki hii na wenzao wa Asia yumkini wakajikuta wana muswada wa pili wa masuala ya uhusiano kati ya nchi na nchi ikiwa ni pamoja na mfarakano kati ya Japani na China na mzozo wa silaha za nuklea wa Korea Kaskazini.

Karibu viongozi 50 wa nchi au serikali watahudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya mkutano wa kwanza wa nchi zinazoendelea huko Bandung Indonesia wakiwemo viongozi wa China, Japani,India,Pakistan,Myanmar na Afrika Kusini.

Agenda rasmi ya mkutano huo wa viongozi wa Asia na Afrika ambao unaanza hapo Ijumaa na kumalizika Jumapili haina utata lakini mazungumzo kati ya nchi na nchi yataangaliwa kwa makini hususan kati ya viongozi wa Japani na China kujadili mzozo juu ya historia ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan atakayehudhuria mkutano huo amewashajiisha Waziri Mkuu wa Japani Junichiro Koizumi na Rais Hu Jintao wa China kuwa na mazungumzo pembezoni mwa mkutano huo.