JAKARTA: Wanamgambo wapata pigo Indonesia
14 Juni 2007Matangazo
Maafisa wa usalama wa Indonesia wamesema wanamgambo wa Kiislamu nchini humo wamepata pigo kubwa kutokana na hatua ya kumtia nguvuni Abu Dujana anayesemekana kuwa kiongozi wa kundi la Jamaah Islamiah.
Maafisa hao wamesema walimkamata Abu Dujana siku ya Jumamosi iliyopita.
Kundi la wanamgambo wa Jamaah Islamiah ndilo linaloshutumiwa kwa kuhusika na mashambuli ya kigaidi ya mwaka 2002 mjini Bali na pia shambulio la bomu la mwaka 2004 dhidi ya ubalozi wa Australia mjini Jakarta.