1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JAKARTA:Waasi wa jimbo la Aceh waanza kukabidhi silaha zao chini ya mpango wa amani.

15 Septemba 2005

Waasi wa zamani wa Indonesia katika jimbo la Aceh,wameanza zoezi la kusalimisha silaha zao chini ya makubaliano ya amani yanaosimamiwa na wasuluhishi kutoka Asia na Ulaya.

Wanachama wa kikundi cha waasi wa zamani cha Free Aceh Movement ama GAM,hadi sasa wamekwishakabidhi silaha 90.Silaha nyingine 800 zitasalimishwa kabla ya kumalizika mwaka huu.

Makubaliano hayo ya mpango wa amani,yaliyotiwa saini mjini Helsinki mwezi uliopita baina ya waasi wa GAM na serikali ya Indonesia,yanalengo la kumaliza vita vilivyodumu miongo mitatu ambavyo vimesababisha maisha ya watu 15,000 kupotea.

Chini ya makubaliano hayo serikali ya Indonesia nayo itapunguza nguvu ya vikosi vyake vilivyopo katika jimbo la Aceh.Katika kutekeleza hayo jana peke yake askari polisi 1,300 waliondolewa katika jimbo hili.

Mpango huo wa amani kwa mujibu wa wadadisi wa mambo,umeongeza matumaini miongoni mwa wananchi wa jimbo la Aceh,ambao bado wanakumbukumbu ya janga la gharika ya Tsunami iliyokumba eneo lao mwezi wa Desemba mwaka jana.

Kwa upande wao waangalizi wa utekelezaji wa makubaliano hayo ya amani kutoka Umoja wa Ulaya,hii ni kazi yao ya kwanza kusimamia upokonywaji wa silaha katika eneo la Asia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW